MABADILIKO YA TAREHE NA VITUO VYA KUFANYIA MITIHANI YA 23 YA BODI

  • Tarehe ya Tukio: Jan 18, 2022 - Jan 21, 2022
  • Muda: 4 DAYS
  • Mahali: COUNTRY WIDE

Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) inapenda kuujulisha umma kuwepo kwa mabadiliko ya tarehe na vituo vya kufanyia mitihani kutoka kwenye mikoa na sasa kufanyika kikanda kama ifuatavyo: Kanda ya Dar es Salaam, Mwanza, Dodoma, Mbeya, Moshi na Unguja - Zanzibar.

Ili kuendana na uteuzi wa watendaji wa Bodi wakiwemo Mwenyekiti na wajumbe wa Bodi na ili kutoa fursa ya ziada ya maandalizi mazuri kwa watahiniwa wa mitihani ya 23, Bodi imesogeza mbele tarehe ya kufanyika kwa mitihani hiyo ambapo sasa mitihani hiyo itafanyika kuanzia tarehe 18.01.2022 mpaka 21.01.2022 badala ya tarehe za awali za kuanzia tarehe 14.12.2021 hadi 17.12.2021 katika kanda zilizoainishwa hapo juu.

Kwa maelezo zaidi bonyeza link

MABADILIKO YA TAREHE NA VITUO VYA KUFANYIA MITIHANI YA 23 YA BODI