PSPTB YAENDESHA MITIHANI YA 30 YA KITAALUMA YA WATAALAM WA UNUNUZI NA UGAVI
Bodi ya wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) imeendesha mitihani yake ya 30 kwa jumla ya watahiniwa zaidi ya 1,000 katika ngazi za Professonal Diploma, Graduate Professional na CPSP. Mitihani hiyo imefanyika katika mikoa Dar es Salaam, Dodoma, Moshi, Arusha, Mbeya, Mwanza na Zanzibar kuanzia terehe 12 hadi 16 May, 2025.
Akizungumza wakati wa mitihani hiyo ikiendelea, Afisa Mitihani kutoka PSPTB Bi. Faraja Mgulambwa amewapongeza wote waliofanikiwa kufanya mitihani hiyo na kwa ushirikiano mkubwa waliouonyesha na kusisitiza juu ya umuhimu wa wahitimu kutoka vyuoni waliosoma fani ya Ununuzi na Ugavi na wale wanaofanya kazi za Ununuzi serikalini na sekta binafsi ila hawana sifa za kitaaluma kuja kufanya mitihani ya Bodi hiyo ili waweze kupata sifa za kitaalam za kufanya kazi za Ununuzi na Ugavi kwa ubobezi na ufanisi zaidi
Bi. Faraja amesistiza zaidi kwamba waajiri wasiajiri watumishi katika eneo la ununuzi na ugavi wasiokuwa na sifa stahiki na hususani wale ambao hawajafanya mitihani ya kitaaluma na kuwa na ujuzi na maarifa stahiki.
“Bodi hii iko macho na hatua stahiki za kisheria na kimaadili zitaendelea kuchukuliwa kwa wale wanaokiuka sheria, kanuni na matakwa ya maadili ya Utendaji kazi iwe ni kwa wataalam wa fani ya Ununuzi na Ugavi au wengine wote wanafanya kazi za ununuzi na ugavi pasipo kuwa sifa kwa kuwa kujisajili na kufanya mitihani hii kumerahishwa sana hivyo nitoe wito kwa wataalam ambao bado hawajafanya mitihani ya bodi kuja kujiandikisha na kufanya mitihani ya bodi mwezi Novemba. Alisema Bw. Ngonyani
Pia amewasisitiza waajiri wenye watumishi wanaopaswa kufanya mitihani ya kitaaluma ili kuwa sifa zinazohitajika kuwapa ruhusa watumishi hao ili waweze kujiendeleza na pia wawalipie ada za mafunzo na za mitihani ili kuwawezesha watumishi hao kufanya mitihani hii muhimu kwa mustakabali wa utendaji wenye tija katika Taasisi zao.