JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi

BARAZA LA WAFANYAKAZI PSPTB LAFANYA TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA BAJETI 2026/27
30 Oct, 2026
BARAZA LA WAFANYAKAZI PSPTB LAFANYA TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA BAJETI 2026/27

Baraza la Wafanyakazi la Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) limekutana jijini Dodoma  Alhamisi, Oktoba 29, 2026, kwa ajili ya kufanya tathmini ya utekelezaji wa bajeti ya taasisi kwa mwaka wa fedha 2026/2027.

Akizungumza katika mkutano huo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB ambaye pia ni Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi na Mwenyekiti wa Baraza hilo, Alex Mfungo, amesema baraza hilo ni la kwanza kwa mwaka wa fedha 2026/2027 na linapitia tathmini ya bajeti pamoja na utekelezaji wa mipango ya taasisi.

Mfungo amesema kuwa kwa kawaida taasisi hufanya mabaraza mawili ya wafanyakazi, ambapo baraza la kwanza hupitia utekelezaji wa bajeti ya mwaka husika, huku baraza lingine likiandaa bajeti ya mwaka unaofuata.

Aidha, amebainisha kuwa wajumbe wa baraza hilo watapata fursa ya kusikiliza mawasilisho kutoka katika idara mbalimbali za taasisi, kuyahoji na kujadili mikakati mingine kwa ajili ya kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa mipango ya taasisi.

Pia ameongeza kuwa utekelezaji wa bajeti kwa robo ya pili ya mwaka wa fedha 2026/2027 unaendelea vizuri, huku kazi zilizopangwa zikiwa zimetekelezwa kwa mujibu wa mpango uliowekwa.

Kwa upande wake, Meneja Rasilimali Watu wa PSPTB, Nancy Mwamakimbula, amesema baraza la wafanyakazi ni muhimu kwa kuwa linafanya tathmini ya yale ambayo taasisi imepanga kuyafanya na mafanikio yake.

Aidha, amesema kuwa baraza hilo pia ni chombo cha maamuzi kinachoangalia masuala muhimu yaliyotekelezwa na kutoa nafasi ya kuhoji na kupata majibu sahihi pale ambapo kuna jambo ambalo halipo sawa.

Aidha, amebainisha kuwa baraza hilo huleta motisha mahali pa kazi kwa watumishi wanapoona mambo yaliyopangwa yametekelezwa na kufanikiwa, huku likiwapa nafasi ya kuzungumza na kuhoji utekelezaji wa mambo mbalimbali.

Pia ameongeza kuwa wajumbe wote wa baraza hilo wana nafasi sawa ya kuhoji masuala mbalimbali bila kuwa na wasiwasi, akisisitiza kuwa chombo hicho kimekuwa na umuhimu katika kupata mafanikio ndani ya taasisi.

 

slot gacor