Matukio katika picha wakati wa Ufunguzi wa wa kongamano la 10 la Ununuzi wa Umma 2026 lililofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC).
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano kwa Umma na Mawasiliano Bi. Shamim Mdee akitoa maelezo kuhusu majukumu ya PSPTB kwa mgeni rasmi Dkt. Toba A. Nguvila (Katibu Tawala Mkoa wa arusha) alipotembelea Banda la PSPTB wakati wa ufunguzi wa kongamano la Ununuzi wa Umma lililofanyika katika ukumbi wa Simba Uliopo AICC jijini Arusha
Naibu Waziri wa Fedha , Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde akipokea maelezo kuhusiana na majukumu ya PSPTB kutoka kwa Mkuu wa Kitengo Cha Uhusiano kwa Umma na Mawasiliano Bi. Shamim Mdee mara alipotembelea banda la PSPTB wakati wa maonesho ya 50 ya kimataifa ya Biashara Sabasaba.
Wananchi mbalimbali wameendelea kutembelea banda la PSPTB katika maonesho ya 50 ya kimataifa ya biashara sabasaba ili kupata elimu juu ya shughuli na majukumu mbalimbali yanayofanywa na PSPTB.
Wananchi mbalimbali wameendelea kutembelea banda la PSPTB katika maonesho ya 50 ya kimataifa ya biashara sabasaba ili kupata elimu juu ya shughuli na majukumu mbalimbali yanayofanywa na PSPTB.
Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB CPSP.Godfred Mbanyi akisaini kitabu cha wageni mara alipotembelea banda la PSPTB katika maonesho ya 50 ya kimataifa ya biashara sabasaba
Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB CPSP.Godfred Mbanyi akipokea maelezo mbalimbali kuhusu huduma zinazotolewa na Ofisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi (TOST) wakati akitembelea mabanda mbalimbali ndani ya jengo la wizara ya Fedha
Mgeni rasmi wa kongamano la 16 la mwaka la wataalam wa ununuzi na ugavi Mhe. Mshamu Munde (katikati) akiwa pamoja na meza kuu wakati wa kongamano hilo lilifanyika katika ukumbi wa AICC jijini Arusha
Graduates of the procurement and supply chain audit course pose for a group photo at the main table during the 14th PSPTB graduation ceremony held at the JNICC hall, Dar es Salaam.
Baadhi ya watahiniwa wa mitihani ya PSPTB wakiwa kwenye chumba cha mitihani wakati wa mitihani hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Suma JKT jijini Dar es salaam.