Biography

Bw. Godfred Mbanyi aliteuliwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mheshimiwa Dk. Phillip Mpango kuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi mnamo tarehe 27 Septemba 2016.

Bw. Mbanyi alijiunga na Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi mwaka 2010 kama Meneja Biashara ya Maendeleo na baadaye kukuzwa na kuwa Mkurugenzi wa Maendeleo ya Taaluma mnamo mwezi Julai 2011 ili kusimamia usajili wa wanataaluma na usimamizi wa kimaadili na kanuni za maadili.

Mnamo mwezi Januari mwaka 2015 alihamishiwa Kurugenzi ya Mafunzo kama Mkurugenzi akiwa na majukumu mahususi ya kusimamia na kuendesha mitihani nafasi aliyokuwa nayo mpaka alipoteuliwa.