KUFANYA MITIHANI YA BODI

MUUNDO WA PROGRAMU YA MITIHANI

1.Utangulizi

Mitihani ya taaluma ya Bodi hufanywa mara mbili kila mwaka yaani, Mei na Novemba na imegawanywa katika ngazi kuu tatu nazo ni Cheti cha Awali, (Basic Stage), Cheti cha Msingi (Foundation Stage) na Shahada ya juu ya Ununuzi na Ugavi (CPSP). Katika kila ngazi za mitihani za mwanzo kila moja ina hatua mbili ambazo zimeundwa kikamilifu ili kupima uelewa, maarifa na ustadi kwa watahiniwa husika katika kufanya kazi za ununuzi na ugavi kuendana na viwango vilivyokusudiwa.

Muundo wa mitihani ya shahada ya juu unazo hatua tano (Professional Stage I - V) zilizoundwa kikamilifu ili kumwezesha mtahiniwa kuwa na maarifa na ujuzi wa kitaalamu ili kuleta tija katika ufanyaji kazi za ununuzi na ugavi katika hatua husika. Kila somo lililomo katika kila hatua za mitihani zilizotajwa humjengea mtahiniwa maarifa na ujuzi ya kumsaidia kuendelea hatua inayofuata.

Kama sehemu ya mtihani, watahiniwa wa ngazi ya juu yaani CPSP baada ya kufaulu mitihani ya hatua ya mwisho (professional stage V) watahitajika kufanya utafiti katika eneo la ununuzi na ugavi na kuwasilisha andiko la utafiti (research paper) kwa Bodi ndani ya kipindi cha miaka miwili kwa ajili ya kusahihishwa.

2.Yaliyomo kwenye muundo wa mitihani ya Bodi

Katika mitihani ya Cheti cha Awali na Cheti cha Msingi kuna jumla ya masomo matano ya msingi (core subjects) na masomo tisa wezeshi (supporting subjects) ambayo yameandaliwa na kuunganishwa kikamilifu ili kuwapa wanafunzi ujuzi na ustadi unaohitajika. Mitihani ya Cheti cha Awali inajumuisha hatua mbili kila moja ikiwa na masomo matatu ambapo ukamilifu wake unakusudia kumuandaa “Technicians” katika kada ya ununuzi na ugavi. Mitihani ya Cheti cha Msingi ina hatua mbili kila moja ina masomo manne, ambapo ukamilifu wake unakusudia kumuandaa “Full Technicians” katika kada ya ununuzi na ugavi.

Kama ilivyoelezwa awali, mitihani ya ngazi ya juu imegawanywa katika hatua tano, zenye masomo kumi na tano (15) ya msingi (core subjects) na masomo matano (5) wezeshi (supporting subjects) na yakifuatiwa na somo moja la kufanya utafiti. Mpango huu umekusudiwa kutoa wahitimu wenye uwezo wa kufanya kazi za ununuzi na ugavi katika viwango vya chini, kati na juu hususani usimamizi wa ununuzi na ugavi.

Kupata ufupisho wa muundo wa mitihani ya PSPTB, tafadhali bonyeza na fungua kiungo hapa chini chenye maelezo mahususi.

PROGRAMU ZA MITIHANI PSPTB

NB: Nakala ngumu ya mtaala inapatikana katika ofisi za PSPTB kwa gharama za Shilingi ya Tanzania 5,000 / =