WATAALAM WA UNUNUZI NA UGAVI WATAKIWA KUZINGATIA WELEDI
WAHITIMU wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) wametakiwa kutumia taaluma yao na kufanya manunuzi kwa kuzingatia weledi, uaminifu na maadili kwani utalitendea taifa haki na kuleta maendeleo.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Jenifa Omolo alieleza hayo jijini Dar es salaam katika mahafali yaliyohusisha wahitimu 368 wa bodi hiyo wakiwemo wataalam wa ngazi ya stashahada, shahada ya kwanza na shahada ya juu ya kitaaluma ya un unuzi na ugavi
Omolo alisema ikiwa wanataaluma watatumia taaluma yao kufanya manunuzi ya kitaalam kwa weledi na kutendea haki maeneo hayo mawili kwa moyo, uaminifu na maadili watatendea taifa haki kwa kuleta maendeleo.
Alisema kwa upande wa serikali na walezi wa kada hiyo wanachukulia suala la weledi kwa uzito kwani limekuwa changamoto kubwa kwenye sekta hiyo ya ununuzi na ugavi.
“Nina Imani wahitimu wa shahada ya juu ya kitaaluma ya ujuzi na ugavi mtaonesha uzalendo na utayari wenu katika kutumikia taaluma na nchi yetu kwa uadilifu na weledi, mwenyezi Mungu awasimamie muweze kutumia viapo mtakavyoapa. amesema Omolo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya PSPTB, Jacob Kibona amesema bodi hiyo imekuwa ikifanya ushirikishwaji wa wadau katika utendaji kazi wake na kwa jitihada na weledi wao wamekuwa na mchango mkubwa katika kuwapata wahitimu hao na waliotangulia.
Naye mmoja wa wahitimu wa masomo ya CPSP, Dominick Abdalah amesema wamejipanga kusaidia taasisi wanazofanyia kazi na jamii kuhakikisha wanafanya manunuzi kwa kuzingatia ubora ili fedha za seriakali katika miradi ikidhi viwango na thamani inayowekwa.